• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan yaripoti watu wanne kuambukizwa kipindupindu katika jimbo la Blue Nile

  (GMT+08:00) 2019-09-10 19:34:28

  Wizara ya afya ya Sudan imetangaza kuwa watu wanne wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu katika jimbo la Blue Nile. Taarifa iliyotolewa na waziri wa afya Bw. Akram Ali Al-Tom, imesema tayari serikali imetoa taarifa kwa Shirika la afya duniani WHO.

  Maofisa wa wawili kutoka wizara ya afya na WHO wamewasili kwenye jimbo la Blue Nile kutoa uungaji mkono kupitia utunzaji wa mazingira, na kuhakikisha usalama wa maji na chakula na matibabu.

  Kuchafuka na kutuama kwa maji kutokana na mvua na mafuriko ni vyanzo vya mara kwa mara vya magonjwa katika baadhi ya maeneo ya Sudan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako