• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapinga waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani kukutana na wafarakanishaji wa Hong Kong

  (GMT+08:00) 2019-09-10 20:00:53

  Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw. Heiko Maas huko Berlin amekutana na Bw. Huang Zhifeng anayejaribu kuitenga Hong Kong kutoka China. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema China inaipinga Ujerumani kuwaruhusu watu wanaojaribu kuitenganisha Hong Kong na China kuingia nchini humo na kufanya shughuli za ufarakanishaji, na kuruhusu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Maas kukutana nao.

  Bibi Hua amesema wiki iliyopita Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel alipofanya ziara nchini China, aliweka bayana kuunga mkono sera ya "Nchi Moja na Mifumo Miwili" na kupinga matumizi ya mabavu. Amesema inabidi kujiuliza Ujerumani ina lengo gani kumruhusu Bw. Huang Zhifeng kufanya shughuli nchini humo na kukutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo. Amesema China inaihimiza Ujerumani ifuate ahadi na kuepusha kutoa ishara ya makosa kwa kundi linalotaka kuitenga Hong Kong kutoka China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako