• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa baraza la kilele la jumuiya ya ushirikiano wa kimataifa ya televisheni ya njia ya hariri wa mwaka 2019 wafunguliwa hapa Beijing

  (GMT+08:00) 2019-09-10 20:04:04

  Mkutano wa baraza la kilele la jumuiya ya ushirikiano wa kimataifa ya televisheni ya njia ya hariri ya mwaka 2019 ulioandaliwa na kituo kikuu cha radio na televisheni cha China na jumuiya ya ushirikiano wa kimataifa ya televisheni ya njia ya Hariri umefanyika hapa Beijing.

  Mkutano huo wenye kaulimbiu ya "Muungano wa Vyombo vya Habari vya aina zote, Maendeleo ya Sifa ya Juu" umehudhuriwa na watu 400 hivi wa ndani na nje, ambao wanaotoka nchi za nje ni pamoja na wakuu wa vyombo 92 vya habari kutoka nchi na sehemu 43.

  Ili kujenga "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kwa sifa ya juu, na kuinua kiwango cha ushirikiano, mkutano huo pia umetangaza kuunda kamati ya jumuiya ya ushirikiano wa kimataifa ya televisheni ya njia ya Hariri, ambayo inaundwa na vyombo vikuu vya habari na mashirika 29 kutoka nchi na sehemu 23 na Mkuu wa kituo kikuu cha radio na televisheni cha China Bw. Shen Haixiong atakuwa mkurugenzi mkuu wa kamati hiyo.

  Bw. Shen ametoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano huo akisema, kituo kikuu cha radio na televisheni cha China kitashirikiana na marafiki wengi zaidi kutoka vyombo vya habari na kuzindua siku nzuri zaidi za mbele za maendeleo ya uvumbuzi ya vyombo vya habari vya dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako