• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanachama wa Baraza la Usalama la UM na Umoja wa Afrika wataka kuondolewa vikwazo nchini Sudan

    (GMT+08:00) 2019-09-11 08:27:38

    Nchi tatu wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika jana waliomba kuondolewa vikwazo vyote vya kimataifa nchini Sudan baada ya nchi hiyo kuunda serikali ya mpito inayoongozwa na raia.

    Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa na balozi wa Cote dÍvoire katika Umoja wa Mataifa Leon Kacou Adom, nchi hizo tatu zikiwemo Cote dÍvoire, Guinea ya Ikweta na Afrika Kusini pamoja na Umoja wa Afrika zimeeleza kutaka kuondolewa kwa vikwazo vyote pamoja na kuiondoa nchi hiyo kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi. Taarifa hiyo pia imeeleza kwamba Baraza la Amani na Usalama la AU limeamua kuondoa vikwazo vilivyoiwekea Sudan vilivyodumu kwa miezi mitatu, kufuatia maendeleo chanya nchini humo.

    Wakati huohuo serikali ya Sudan imetangaza vipaumbele 10 vya kutekelezwa katika siku 200 za mwanzo katika kipindi cha serikali ya mpito. Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni pamoja na kusitisha vita, kujenga amani, kukabiliana na msukosuko wa uchumi, kuongeza haki za wanawake, kuunda tena taasisi za kitaifa na kupambana na ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako