• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RAGA: KCB bingwa wa Raga wachezaji 7 kila upande

  (GMT+08:00) 2019-09-11 08:58:41

  Mashindano ya raga ya kitaifa ya wachezaji 7 kila upande nchini Kenya yamekamilika huku timu ya KCB ikiibuka bingwa wa michuano hiyo baada ya ukame wa miaka minne mfululizo wa kutonyakua taji hilo.

  Vijana hao wa kocha Dennis Mwanja, walitoka nyuma bila alama wakati wa mapumziko katika mechi hiyo na kuduwaza Impala inayofundishwa na kocha Oscar Osir na kumaliza msimu huu wa ligi hiyo ya raga kwa alama 116.

  Timu ya Mwamba yenyewe imemaliza katika nafasi ya pili kwa kupata alama 92. Huku Homeboyz wao imekamata nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 90.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako