• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Harambee Stars yashindwa kufurukuta nyumbani, yatoka sare na Uganda Cranes

  (GMT+08:00) 2019-09-11 08:57:44
  Wiki tatu baada ya uteuzi wa Francis Kimanzi kuongoza timu ya taifa ya soka ya Kenya almaarufu Harambee Stars kuonekana kugawanya Wakenya, mashabiki mnamo Jumapili walikuwa wakiimba wimbo mmoja wakimmiminia sifa kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya Uganda (Uganda Cranes).

  Majirani hao walikabana koo katika mechi safi ya kirafiki uwanjani Kasarani, ambayo Mganda Emmanuel Okwi alipeleka timu yake mapumzikoni ikiwa kifua mbele kabla ya Kenneth Muguna kusawazishia wenyeji katika kipindi cha pili.

  Mashabiki wengi wanasema sare ni mwanzo mwema kwa Kimanzi, ingawa wamemtaka Stars kuimarika katika mechi zijazo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako