• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na wajumbe wa makampuni ya Marekani

    (GMT+08:00) 2019-09-11 09:39:47

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amekutana na wajumbe wa Marekani waliohudhuria mazungumzo kati ya wanaviwanda wa China na Marekani.

    Bw. Li amesema huu ni mwaka wa 40 tangu China na Marekani zianzishe uhusiano wa kibalozi, na katika miaka 40 iliyopita, uhusiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo umeendelea kwa mfululizo na kuleta manufaa ya pamoja. Amesisitiza kuwa China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, na Marekani ni nchi kubwa zaidi iliyoendelea, zina maslahi mengi ya pamoja, pande hizo mbili zinapaswa kufuata makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wao, na kanuni ya usawa na kuheshimiana, kutafuta maoni ya pamoja, na kuvumilia maoni tofauti, ili kutatua mvutano kwa njia inayokubaliwa na pande zote.

    Aidha, Bw. Li amesema China ina soko kubwa, na inakaribisha makampuni ya nchi za nje ikiwemo Marekani kupanua ushirikiano na China, ili kupata mafanikio ya pamoja.

    Wajumbe wa Marekani wameeleza matumaini yao kuwa mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili yatapiga hatua, na kufikia makubaliano mapema iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako