• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ofisa wa Afrika Kusini asema matukio ya kimabavu ya karibuni si vitendo vya chuki dhidi ya wageni

  (GMT+08:00) 2019-09-11 09:49:05

  Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula amesema, matukio ya kimabavu yaliyoanza kutokea mwishoni mwa mwezi uliopita na kudumu hadi sasa nchini humo si vitendo vya chuki dhidi ya wageni.

  Akilihutubia bunge la Afrika Kusini jana mjini Cape Town, Mapisa-Nqakula alisema, migogoro ya kimabavu ya karibuni ilisababisha vifo vya watu 12 wakiwemo waafrika kusini 10. Katika kipindi cha migogoro, maduka mengi yaliyoendeshwa na Waafrika kusini yaliporwa na kuharibiwa.

  Mapisa-Nqakula amebainisha kuwa, katika kipindi cha migogoro ya kimabavu, wageni 755 walikwenda idara mbalimbali za polisi kutafuta ulinzi. Serikali ya Afrika Kusini inafanya juhudi ya kuwapatia misaada ya kibinadamu watu hao, pia inawasiliana na balozi za nchi mbalimbali, na kuwasaidia wadau husika warudi nyumbani kwao haraka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako