• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la 5 la uwekezaji Afrika lazingatia uanuwai wa uchumi na utoaji wa nafasi za ajira

    (GMT+08:00) 2019-09-11 09:58:02

    Kongamano la 5 la uwekezaji barani Afrika limefunguliwa jana huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, na kuangalia kwa kina ushirikiano kwa uchumi anuwai na utoaji wa nafasi za ajira kwenye uchumi wa Afrika.

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesema, kongamano hilo linafanyika katika wakati muafaka kwani bara hilo liko katika kipindi muhimu cha kutekeleza makubaliano ya maeneo ya biashara huria ya Afrika AfCFTA, ambayo yanalenga kuhimiza utandawazi na maendeleo ya uchumi.

    Amesema mada za kongamano hilo ni muhimu katika kutimiza lengo hilo na kongamano hilo litasaidia kuongeza kuvutia uwekezaji kuja Afrika.

    Rais Denis Sassou Nguesso wa Kongo amesema, uwekezaji kutoka China umechangia sana kwenye maendeleo ya uchumi barani Afrika, na kutaka kuimarisha ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika katika sekta za teknolojia ya kidigitali na ujenzi wa miundo mbinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako