• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkuu wa CMG akutana na viongozi wa mashirika ya habari ya Reuters na AP

  (GMT+08:00) 2019-09-11 10:22:14

  Mkurugenzi mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Bw. Shen Haixiong jana kwa nyakati tofauti alikutana na mkurugenzi wa Shirika la habari la Uingereza Thomson Reuters Bw. Michael Friedenberg na ofisa mwandamizi wa shirika la habari la Marekani AP (Associated Press) Bw. Brad Foss.

  Akikutana na mwenzake wa Reuters, Bw. Shen Haixiong amesema Shirika la habari la Thomson Reuters ni chombo maarufu cha habari duniani, na habari zake za kifedha zina ushawishi mkubwa kwenye sekta hiyo. Amesema uhalisi, ukweli na haki ni vigezo vya kimsingi ambavyo CMG siku zote linavifuata kwenye kazi za utangazaji na uandishi wa habari, na CMG linapenda kuimarisha ushirikiano na Reuters katika kubadilishana taarifa za habari na kuripoti matukio makubwa, ili kuelekeza maoni ya umma kwa sauti za haki.

  Kwa upande wake Bw. Friedenberg amesema anakubali maoni ya Bw. Shen, na kusema Reuters inatilia maanani ushirikiano kati yake na CMG, haswa kwenye utoaji habari na huduma za kifedha, na pia inatarajia kukamilisha utaratibu wa mawasiliano na CMG.

  Alipokutana na Bw. Brad Foss, Bw. Shen Haixiong amesema CMG na AP zimekuwa na ushirikiano wenye ufanisi katika ujenzi wa vituo vya CMG katika nchi za nje, utoaji habari za kimataifa kwa lugha mbalimbali na ujenzi wa mtandao wa utoaji habari wa kimataifa. Amesema katika hatua ijayo, CMG itaendelea kuimarisha ushirikiano na mawasiliano na AP, kwenye msingi wa kusaidiana na kunufaishana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako