• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatangaza orodha ya bidhaa za Marekani ambazo hazitaongezwa ushuru ili kupunguza athari mbaya kwa makampuni ya kigeni nchini China

  (GMT+08:00) 2019-09-11 17:02:25

  Kamati ya kanuni ya ushuru kwenye Baraza la Serikali la China imetangaza orodha ya awamu ya kwanza ya bidhaa za Marekani ambazo zitasamehewa kuongezwa ushuru, ambayo utekelezaji wake utaanza rasmi Septemba 17 mwaka 2019. Hii ni mara ya kwanza kwa China kutangaza orodha ya aina hiyo tokea Marekani ilipochochea na kupandisha mgogoro wa uchumi na biashara. Lengo la hatua hii ni kupunguza athari mbaya zinazotokana na mgogoro huo dhidi ya makampuni ya kigeni nchini China, ambayo imeonesha msimamo wa kujizuia, na wa kimantiki wa China katika kukabiliana na mgogoro huo, na kuwajibika kwa makampuni na wananchi.

  Katika mwaka mmoja uliopita, kutokana na kukabiliwa na vitendo vya Marekani vya utaratibu wa upande mmoja, na kujilinda kibiashara, China ililazimika kulipiza kisasi kwa raundi tatu. Hatua ya China ya kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani hailengi kuyatoza ushuru makampuni, bali ni kulinda kithabiti maslahi makuu ya nchi na maslahi ya kimsingi ya wananchi, na kulinda maslahi yake halali ya kujiendeleza. China inafahamu vizuri kwamba, hamna mshindi katika vita vya biashara, hatua ya kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za Marekani vilevile italeta athari mbaya kwa baadhi ya makampuni nchini China. Ndiyo maana China inapinga kithabiti kupandisha vita vya biashara. Wakati inapochukua hatua ya kukabiliana na umwamba wa kibiashara wa Marekani, pia itafanya juhudi za kupunguza mapigo dhidi ya makampuni ya kigeni nchini China. Na orodha hii ya baadhi ya bidhaa za Marekani kusamehewa ushuru imeonesha vya kutosha msimamo huo wa China.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na China, katika muda wa mwaka mmoja tangu kutekelezwa kwa orodha hiyo, China haitatoza tena ushuru dhidi ya bidhaa zinazoorodheshwa, na kurejesha ushuru kwa bidhaa zinazokidhi masharti yanayohusika. Hali ambayo imeonesha unyumbufu wa utatuzi wa matatizo wa China juu ya masuala halisi.

  Tokea mgogoro wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani ulipotokea mwezi Machi mwaka jana, China imekuwa ikitathmini athari mbaya zinazoyakabili makampuni mbalimbali, na kuchukua hatua ili kupunguza shinikizo hilo Utoaji wa orodha hiyo umeonesha kuwa sera za China za kukabiliana na mgogoro wa uchumi na biashara zimekamilika zaidi. Katika kipindi kijacho, idara zinazohusika za China zitaendelea na hatua ya kusamehe ushuru bidhaa za Marekani, na kutangaza orodha nyingi zaidi. Hayo yameonesha kuwa, bidhaa nyingi zaidi zinazoagizwa kutoka Marekani hazitaongezwa ushuru, na China itaendelea kufanya juhudi za kupunguza athari mbaya zinazotokana na mgogoro wa uchumi na biashara kwa makampuni ya kigeni nchini China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako