• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China atangaza amri ya kumteua He Yicheng kuwa mkuu wa awamu ya tano wa mkoa wa utawala maalum wa Macau

  (GMT+08:00) 2019-09-11 19:33:35

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang hapa Beijing amekutana na Bw. He Yicheng na kutangaza amri ya kumteua kuwa mkuu wa awamu ya tano wa mkoa wa utawala maalum wa Macau.

  Bw. Li amesisitiza huu ni mwaka wa 20 tangu Macau irudi China, na serikali kuu itaendelea kutekeleza kwa pande zote sera ya "Nchi Moja na Mifumo Miwili", "Wamacau kuitawala Macau", mwongozo wa kujitawala wa kiwango cha juu na kutawala kwa mujibu wa katiba na sheria ya kimsingi, huku ikiunga mkono kwa nguvu zote awamu mpya ya serikali ya mkoa wa utawala maalum wa Macau kutekeleza sera kwa kufuata sheria na utawala bora.

  Bw. He amesema baada ya kuingia madarakani atatekeleza kithabiti sera ya "Nchi Moja na Mifumo Miwili", kutawala kwa kufuata katiba na sheria za msingi, na kufanya juhudi kuhimiza maendeleo ya pande nyingi ya Macau, kuboresha maisha ya umma na kushiriki kwenye ujenzi wa eneo kubwa la ghuba la Guangdong-Hong Kong na Macau.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako