• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawataka baadhi ya wamarekani kutoingilia mambo ya Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-09-11 19:33:52

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inawataka baadhi ya wamarekani kutoendelea kujifanya wanasinzia na kufumbia macho vitendo vya uhalifu na mabavu kwa makusudi, na kuacha kuingilia kati mambo ya Hong Kong.

    Habari zinasema baadhi ya wabunge wa Marekani wametangaza kuwa watatoa pendekezo la kusimamisha kuuza vifaa vya utekelezaji wa sheria kwa Hong Kong.

    Bibi Hua amesisitiza kuwa kwa upande mmoja baadhi ya wabunge wa Marekani wamesifu uhalifu na mabavu kama kupigania haki za binadamu na uhuru. Kwa upande mmoja wamewachafua polisi wa Hong Kong wanaojizuia kutekeleza sheria kama watu wanaotumia mabavu kupita kiasi. Huku ni kuchafua uhuru, demokrasia na haki za kibinadamu, na ni dharau kwa maoni ya umma ya Hong Kong, kuhusu kuzuia mabavu na kurejesha utaratibu, na umeonesha unafiki wao na vigezo viwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako