• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya yalenga kuuza zaidi nchini China

    (GMT+08:00) 2019-09-11 19:40:58
    Kenya inapanga kuongeza uuzaji wake wa bidhaa kwenda soko la China kwa kuandaa hafla za uendelezaji.

    Hivi karibuni matukio kadhaa yalifanyika katika mji mkuu Beijing kati ya Agosti 30 na Septemba 3 kukuza bidhaa za Kenya.

    Wakati wa maonyesho ya Kilimo ya Kimataifa yaliofanyika mjini humo Kenya pia imeonesha bidhaa zake za huduma kama vile utalii, biashara na uwekezaji kupitia Kituo cha kukuza Utamaduni na Biashara ya Kenya.

    Katibu wa kudumu wa wizara ya Biashara wa Kenya Chris Kiptoo alisema Kenya inategemea uhusiano mzuri na China ili kuongeza mauzo ya nje kwenda Beijing kwa asilimia 20 kila mwaka.

    Alisema mnamo 2018, mauzo ya Kenya kwenda China yaliongezeka kwa asilimia 10 na mwaka 2019 yanatarajiwa kufikia asilimia 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako