• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Cameroon atoa mwito wa kuwepo kwa mjadala wa kitaifa ili kukomesha mgogoro kwenye eneo wanalotumia Kiingereza

  (GMT+08:00) 2019-09-11 19:41:46

  Rais Paul Biya wa Cameroon ametoa mwito wa kuwepo kwa mjadala wa kitaifa ili kutatua msukosuko ulioyakumba majimbo mawili ya nchi hiyo yanayotumia lugha ya kiingereza ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi.

  Mazungumzo hayo yanapangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, na yatalenga kukidhi matarajio ya watu wa majimbo hayo. Waziri Mkuu wa Cameroon Bw. Joseph Dion Ngute ataendesha mkutano huo utakaowakutanisha maofisa wa serikali na wawakilishi wa makundi ya wanaotaka kujitenga.

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amekaribisha wito wa Rais Biya, na kuuhimiza serikali ya Cameroon kuhakikisha kuwa mchakato wa majadiliano unakuwa shirikishi na unashughulikia changamoto zinazoikabili nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako