• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Mitwa Ng'ambi kuwa mkurungezi mkuu mpya wa MTN Rwanda

  (GMT+08:00) 2019-09-11 19:41:55
  Kampuni ya mawasiliano ya MTN tawi la Rwanda inatarajiwa kupata mkurungezi mkuu mpya mwezi huu. MTN inasema mkuu wake mpya atakuwa ni Mitwa Kaemba Ng'ambi akichukua mahali pa Bart Hofker ambaye ameongoza kampuni hiyo tangu 2016.

  Bart anaelekea Zambia ambako atakuwa mkurungezi mkuu baada ya kuondoka kwa mkuu wa sasa Philip van Dalsen, mwishoni mwa mwezi.

  Ng'ambi amefanya kazi kwenye sekta ya mawasiliano ya simu kwa zaidi ya miaka 10.

  Amekuwa akifanya kazi kama mkurungezi mkuu Airtel-Tigo nchini Ghana.

  Ana Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Joensuu, Ufini, na Shahada ya Sayansi katika Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Namibia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako