• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kazi ya kurefusha reli ya SGR nchini Kenya inakaribia kukamilika

  (GMT+08:00) 2019-09-11 19:42:09

  Awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya SGR inayounganisha mji wa Nairobi na mji wa Naivasha imeingia hatua ya mwisho, na majaribio ya mwezi mmoja yameanza mwezi huu.

  Reli hiyo yenye urefu wa kilometa 120 ni sehemu ya mtandao wa reli SGR kutoka Mombasa hadi Nairobi. Mpaka sasa kazi kubwa za ujenzi zimekamilika ikiwa ni pamoja na kutandika reli na kujenga vituo vitano, na kazi ya kukamilisha wigo na alama za kuongoza treni inaendelea. Daraja lenye urefu wa kilometa 6.5 limejengwa kwenye mbuga ya wanyama ya Nairobi, ili kuhakikisha ujenzi wa reli hiyo hauharibu mazingira ya asili ya wanyama.

  Zaidi ya vijana 500 wamenufaika kwa kupata ajira katika ujenzi wa reli hiyo, ambayo inatarajiwa kuwa na matokeo chanya kwenye sekta za kimkakati za Kenya kama vile kilimo, utalii na viwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako