• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mfumko wa bei wapungua Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-09-11 19:42:14
    Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania (NBS) imetangaza kupungua kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka unaoishia Agosti 2019 hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka unaoishia Julai 2019.

    Kaimu mkurugenzi wa takwimu za sensa na kijamii, Ruth Davison amesema hiyo inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bidhaa na bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Agosti, 2019 imepungua ikilinganisha na kasi iliyokuwepo kwa mwaka unaoishia Julai, 2019.

    Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Agosti 2019 zikilinganishwa na bei za Agosti 2018.

    Amesema baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizopungua bei kwa Agosti 2019 zikilinganishwa na bei za Agosti 2018 ni mafuta ya taa kwa asilimia 2.6 na petroli kwa asilimia 4.3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako