• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya Dunia yazitaka nchi za Afrika zifanye maamuzi thabiti kuhusu mageuzi ya kidigitali

  (GMT+08:00) 2019-09-11 19:42:32

  Benki ya Dunia imesema nchi za Afrika zinatakiwa kufanya maamuzi thabiti kuhusu mageuzi ya kidigitali, kwa kuwekeza kwenye miundo mbinu ya kidigitali, ili ziweze kufikia malengo ya Umoja wa Afrika ya huduma za internet kwa wote na kwa gharama nafuu.

  Kwenye mkutano wa tano wa baraza la uwekezaji barani Afrika unaoendelea mjini Brazzaville, imefahamika kuwa huduma za internet yenye kasi, zinasaidia kutoa nafasi za ajira kwa makundi yote ya elimu. Ripoti yenye kauli mbiu ya teknolojia za kidigitali kwa wote barani Afrika, imesisitiza umuhimu wa kuwapa wafanyakazi ujuzi wa kidigitali na kutatua tatizo la kuwa na ujuzi wa kimsingi wa teknolojia za kidigitali.

  Kwenye mkutano huo wa siku tatu ulioandaliwa kwa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kongo, Wizara ta Fedha ya China, Benki ya Maendeleo ya China na Benki ya Dunia, Benki ya Dunia imesema nchi za Afrika zinatakiwa kuchukua hatua sasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako