• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Samatta asubiri majibu ya MRI

  (GMT+08:00) 2019-09-12 08:11:36

  Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, amefanyiwa uchunguzi wa goti aliloumia wakati akiiongoza taifa stars dhidi ya Burundi katika mchezo wa marudiano uliochezwa jijini Dar es Salaam.

  Samatta aliyefunga goli la kuongoza kwa Stars kabla ya Burundi kusawazisha kisha kwenda kwenye matuta, alipata majeraha ya goti ambayo yalimlazimu kaimu kocha wa taifa stars Suleman Matola ampumzishe na nafasi yake kuchukuliwa na Himid Mao. Mara baada ya kurejea Ubelgiji, klabu yake ya Genk imeamua kumfanyia uchunguzi zaidi licha ya yeye mwenyewe kuona hana maumivu makubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako