• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yasema reli ya SGR iliyojengwa na China hataathiri sekta ya usafirishaji wa mizigo barabarani

  (GMT+08:00) 2019-09-12 08:47:30

  Kenya imesema uendeshaji wa reli ya SGR inayotoka Mombasa hadi Nairobi ambayo imejengwa na China unaendelea kuboresha usafirishaji wa mizigo na abiria na hautaathiri sekta ya usafirishaji mizigo barabarani.

  Akiongea mjini Nairobi, waziri wa uchukuzi, miundombinu, nyumba na maendeleo ya miji wa Kenya James Macharia amesema ingawa reli ya SGR inatumika kwa ukamilifu, lakini inasafirisha asilimia 40 tu ya mizigo inayopitia bandari ya Mombasa na kubakisha asilimia 60 kusafirishwa kwa njia ya barabara. Hivyo waziri Macharia amesisitiza kuwa kinyume na wasiwasi walioonesha wadau, SGR haitaua usafiri wa barabarani bali inachangia kutoa wepesi wa kusafirisha abiria na mizigo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako