• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Alibaba yazindua progranmu ya biashara ya mtandaoni kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza wa Afrika

  (GMT+08:00) 2019-09-12 08:47:58

  Kampuni kubwa ya biashara ya China Alibaba jana ilizindua programu yake ya kwanza ya biashara ya kuvuka mipaka kwenye mtandao kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza wa Afrika.

  Wanafunzi 22 kutoka Rwanda Jumanne waliwasili katika mji wa Hangzhou, yaliyopo makao makuu ya Alibaba, ikiwa inaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. Akiongea kwenye sherehe za ufunguzi mkurugenzi wa Chuo cha Biashara katika Chuo kikuu cha Ualimu cha Hangzhou, Zeng Ming amesema chuo hicho sio cha biashara ya jadi bali kinazingatia uchumi kwenye mtandao wa internet. Amefafanua kuwa wanafunzi wa kigeni wanaweza kuchukua kozi zinazohusiana na internet, biashara ya kimataifa na biashara ya kuvuka mipaka kwenye mtandao na pia kupata uzoefu wa kwanza wa maendeleo ya uchumi wa kidijitali wa China.

  Mradi huo ni sehemu ya makubaliano ya ushirikiano kati ya serikali ya Rwanda na Alibaba chini ya mpango wa pili wa Jukwaa la Biashara kwenye Mtandao Duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako