• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya Umoja wa Mataifa yatoa wito wa kubadili mwelekeo wa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu

    (GMT+08:00) 2019-09-12 08:48:30

    Umoja wa Mataifa jana ulitoa ripoti mpya ukisema Kukuza uchumi kwa kuongeza matumizi ya maliasili sio tena njia yenye mafanikio katika ngazi ya kimataifa.

    Ripoti hiyo iliyozitaka nchi zote kutathmini maendeleo ya Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030, ni ya kwanza ya aina yake tangu kupitishwa kwa malengo ya Maendeleo Endelevu miaka minne iliyopita. Ripoti hiyo iliyoandikwa na jopo la wanasayansi walioteuliwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, inatarajiwa kuwasilishwa katika Kongamano la Ngazi ya Juu la Kisiasa katika Mkutano wa Kilele wa Maendeleo Endelevu wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika Septemba 24 na 25 huko New York.

    Kulingana na ripoti, kuendeleza uchumi kupitia matumizi kunafanya maliasili zizidiwe duniani na kupelekea maliasili zenye sumu ambazo zinatishia kuelemewa kwa dunia. Hivyo wanasayansi wameshauri ulimwengu lazima ubadilishe maeneo muhimu ya shughuli za binadamu, ikiwemo chakula, nishati, matumizi na uzalishaji, na miji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako