• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa usambazaji wa maji wa Zambia unaojengwa na China wamalizika kwa asilimia 55

    (GMT+08:00) 2019-09-12 09:15:57

    Ujenzi wa mradi wa mfumo wa usambazaji wa maji wa Kafulafuta wa Zambia unaogharimu dola za Marekani milioni 449 na kujengwa na kampuni ya CNCEC ya China, umemalizika kwa asilimia 55.

    Afisa mahusiano ya umma wa wizara ya maji na maendeleo ya usafi wa mazingira Bw. Amos Zulu amesema, mradi huo unaolenga kuongeza usambazaji wa maji katika wilaya za Ndola, Luanshya, Mpongwe na Masaiti, utanufaisha watu laki 7. Pia amesema, baada ya mradi huo kukamilika utaongeza muda wa usambazaji wa maji kutoka saa 18 hadi saa 24 kwa siku na kupunguza ukosefu wa maji kutoka asilimia 64 hadi asilimia 35.

    Habari zinasema, mradi huo ulioanza kujengwa Septemba, mwaka jana, unatarajiwa kukamilika mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako