• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Sudan Kusini waahidi kutimiza amani

    (GMT+08:00) 2019-09-12 09:16:11

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na mpinzani wake Bw. Riek Machar wamepongeza mafanikio yaliyopatikana katika kutatua changamoto kubwa zinazokabili utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa Septemba, mwaka jana.

    Baada ya kukutana mjini Juba, viongozi hao wawili wamesema wamechagua kufuata njia ya amani na wana imani kuwa, makubaliano hayo yatasaidia kutatua masuala magumu kati yao, kama vile, mpango wa usalama na idadi ya majimbo kabla ya kuunda serikali ya umoja Novemba, mwaka huu.

    Rais Kiir amesema, mazungumzo yake na Bw. Riek Machar yamekwenda vizuri. Pande hizo mbili zinaweza kufikia makubaliano ya kuelewana na kutarajia kutatua matatizo yaliyopo mapema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako