• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwili wa Mugabe wafika Zimbabwe kabla ya mazishi Jumapili

  (GMT+08:00) 2019-09-12 09:18:45

  Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, aliyekufa nchini Singapore Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 95, umefika Zimbabwe jana Jumatano alasiri kabla ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika Jumapili. Wanasiasa akiwemo rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na mamia ya raia wamepokea mwili wa Mugabe kwenye uwanja wa ndege.

  Katika shughuli ya mapokezi katika uwanja wa ndege rais Mnangagwa alitoa risala akisifu maisha ya marehemu Mugabe, na kumwita baba wa taifa, mwalimu wa mapinduzi na nguzo ya Umoja wa Afrika.

  Rais Mnangagwa amesema, serikali ya Zimbabwe itauaga mwili wa Mugabe kitaifa tarehe 14 kwenye uwanja wa michezo wa kitaifa kabla ya mazishi yatakayofanyika Septemba 15.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako