• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwakilishi wa wanawake Hongkong asema wanaojidai kuwa ni "wapiganaji wa uhuru" ni wanafiki wanaotumia vigezo viwili

  (GMT+08:00) 2019-09-12 09:29:16

  Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanawake la Hongkong Bi. Pansy Ho Chiu-king amesema wale wanaojidai kuwa ni "wapiganaji wa uhuru" mkoani Hongkong ni wanafiki na wanatumia vigezo viwili.

  Akizungumza kwenye kikao cha 42 cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea huko Geneva, Bi. Ho amesema yeye na familia yake walishambuliwa, kudhalilishwa na kutishiwa kwenye mtandao wa Internet na wale wanaojidai kuwa ni wapiganaji wa uhuru ambao wanajificha nyuma ya mask na kutothubutu kutaja majina yao ya kweli. Amesema vitendo hivyo ni njia ovu ya kueneza kitu kisicho na msingi wanachoshikilia kuwa ni ukweli.

  Amekiambia kikao hicho kuwa katika siku zilizopita, wakazi wengi wa kawaida wa Hongkong wamekabiliwa na mabavu ya aina mbalimbali, kimwili na kiakili.

  Bi. Ho pia amsema mbali na vitendo vya kuchoma moto, kuharibu mali na miundombinu ya usafiri wa umma, kushambulia polisi na raia wasio na hatia, watu hao wenye itikadi kali pia walitumia vyombo vya habari na mtandao kuvamia faragha za watu, kueneza habari feki na za kupotosha ili kuchochea mashaka na hofu katika jamii, na hatimaye kutoa visingizio kwa vitendo vyao vya kimabavu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako