• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Sudan na makundi ya wapiganaji wakubaliana kufanya mazungumzo ya amani mwezi ujao

  (GMT+08:00) 2019-09-12 10:16:34

  Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na baraza la utawala nchini Sudan, Serikali ya Sudan na makundi ya wapiganaji wamekubaliana kufanya mazungumzo ya amani Oktoba, 14. Tangazo hilo lilitolewa baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Juba kati ya wawakilishi wa serikali ya Sudan na makundi ya wapiganaji yanayotoka majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile, kufuatia pendekezo la upatanishi lililotolewa na rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini. Pande hizo pia zimekubali kuunda kamati maalumu za kupanga mazungumzo ya amani, kufuatilia utaratibu wa kuwaachia huru wahalifu wa kivita na wafungwa, kushughulikia hatua za kumaliza uhasama na kuidhinisha utaratibu wa usimamizi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako