• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viongozi wa nchi 11 wathibitisha kuhudhuria mazishi ya Bw. Mugabe

  (GMT+08:00) 2019-09-12 19:41:48

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema hadi sasa viongozi wa nchi 11 wamethibitisha kuwa watahudhuria shughuli ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, itakayofanyika Jumamosi katika uwanja wa taifa.

  Bw, Mnangagwa amesema hayo akiambatana na wajumbe waandamizi ya chama cha ZANU-PF na wa idara nyingine, alipokwenda kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya Bw. Mugabe nyumbani kwake. Pia amesema atajadiliana na mjane wa marehemu Bibi Grace, kuhusu siku na mahali pa mazishi.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying, amesema mjumbe maalum wa Rais wa China Bw Gu Shengzu atahudhuria shughuli ya mazishi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako