• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais za Dk Shein aupongeza ushirikiano wa Zanzibar na China

    (GMT+08:00) 2019-09-12 19:53:58
    Rais wa Zanzibar ,Dk Ali Mohamed Shein,ameipongeza China kwa kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha maendeleo ikiwamo kuipatia wataalamu kwa ajili ya kuwafunza wazanzibari.

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alisema hayo ikulu mjini Zanzibar wakati alipokutana na kuzungumza na Katibu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),Dong Weihong,ambaye ni Makamu Mkuu wa Taasisi ya China National Research Institute of Food Fermentation Industries ya China.

    Katika mazungumzo hayo,Dk shein alisema kuwa Jamhuri ya watu wa China na Zanzibar zina historia ndefu ya ushirikiano.

    Alisema China inaleta wataalamu na wakufunzi wake Zanzibar katika sekta mbalimbali zikiwamo afya,kilimo,viwanda na elimu.

    Alisema kuwa juhudi hizo zina manufaa makubwa kwa sasa na baadaye kwani ni kivutio kimojawapo cha kupanua wigo wa masuala ya kuvutia watalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako