• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • ULAMA: Mpira wa Mawe kurudi kwa kishindo nchini Mexico

  (GMT+08:00) 2019-09-13 07:51:07

  Kundi la vijana wa Mexico linafufua mchezo wa jadi wa mpira wa mawe kwao maarufu kama 'Ulama', uliowahi kuchezwa na jamii za Aztecs, Maya na Incas.

  Katika mchezo huo wachezaji huvaa mikanda maalumu na vitamba vya kujifunika na wanasukuma mpira kwa viuno vyao. Mpira unatajwa kuweza kuwa na uzito wa hadi kilo 4 na inaaminika kuwa kuna aina tofauti za mchezo huo na mara nyingi ilidhaniwa ulihusisha timu hasimu zikikabiliana ana kwa ana.

  Emmanuel Kakaloti mkufunzi wa mchezo huo amesema Ulama ulisahaulika na kuachwa kuchezwa lakini sasa wanaurudisha na kutakuwa na timu ya wanawake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako