• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA YA MAREKANI: Antonio Brown ashtakiwa kumbaka kocha wake

  (GMT+08:00) 2019-09-13 07:51:55
  Mchezaji wa klabu ya New England Patriots ya Marekani Antonio Brown, ameingia kwenye utata mpya baada ya kutuhumiwa kumbaka kocha wake wa zamani na kufunguliwa mashtaka jijini Florida Marekani.

  Brown ambaye mwishoni mwa wikiendi alisajiliwa na mabingwa hao wa Super Bowl baada ya kuruhusiwa na Oakland Raiders, anatuhumiwa kumbaka mwalimu wake huyo mwenye umri wa miaka 28 katika matukio matatu tofauti yaliyotokea mwaka 2017 na 2018.

  Klabu yake ya Patriots imesema, imepokea taarifa hizo na kusema inazichukua kwa uzito mkubwa na kuwa klabu hiyo hairuhusu mashambulisi ya kingono, hivyo wanasubiri mamlaka husika zikamilishe uchunguzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako