• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Chepkoech aongoza watatu kuingia riadha ya dunia mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji

  (GMT+08:00) 2019-09-13 07:53:50
  bingwa mtetezi wa mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji wa Kenya Beatrice Chepkoech ameshinda kiurahisi kitengo chake kwenye mashindano ya kuchagua timu itakayopeperusha bendera ya Kenya kwenye mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika jijini Doha nchini Qatar Septemba 27 hadi Oktoba 6 mwaka huu.

  Mchujo huo ulianzia uwanja wa Nyayo jijini Nairobi jana, huku Beatrice akikamilisha mizunguko 28 na kuruka maji mara 7 kwa 9:45:15 akifuatiwa kwa karibu na bingwa wa mwaka 2015 Hyvin Kiyeng aliyetumia 9:45:20.

  Kenya inaruhusiwa kuingiza wanariadha wanne katika kitengo hicho kwasababu Chepkoech alishinda mashindano ya Diamond League.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako