• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNHCR latoa wito kwa mataifa ya Afrika kusaini mkataba wa wakimbizi na kuutekeleza kikamilifu

  (GMT+08:00) 2019-09-13 08:11:27

  Wakati mkataba wa wakimbizi wa Afrika ukifikisha miaka 50, Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa wito kwa mataifa ya Afrika ambayo bado hayajasaini mkataba huo ku saini, na yaliyosaini kuutekeleza kikamilifu.

  Kwenye taarifa yake shirika hilo limekaribisha hatua muhimu za mkataba huo uliopitishwa Septemba 10, 1969 yakiwa kama makubaliano ya kwanza duniani ya kuwalinda wakimbizi katika kanda hiyo na yanayoikamilisha kanda kwenye Mkataba wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1951. Mkataba huo uliosaniwa na nchi 47 kati ya nchi 55 za Umoja wa Afrika, wiki hii unatimiza miaka 50.

  Mwakilishi wa UNHCR katika Umoja wa Afrika Cosmas Chanda amesema ni mkataba ulioleta maendeleo na kupanua maana ya wakimbizi ambao umeendelea kufaa katika nusu karne. Chanda amekaribisha hatua ya hivi karibuni ya Rwanda kuwasaidia wakimbizi na watafuta hifadhi kutoka Libya ikiwa ni ishara ya kuenzi maadhimisho ya mkataba wa wakimbizi wa mwaka 1969.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako