• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya UM yasema misukosuko ya kibinadamu imekithiri mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2019-09-13 08:53:42

    Ripoti ya mwaka 2018 iliyowasilishwa na Baraza la Usalama kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa inasema misukosuko mikubwa ya kibinadamu imeendelea duniani na baadhi yao kimekithiri zaidi, ambapo watu wengi zaidi walikimbia makazi yao ndani na nje ya nchi kutokana na vurugu na machafuko.

    Ripoti hiyo mpya iliyojadiliwa kwenye kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wiki hii, inasema Baraza la Usalama lilipitisha maazimio 54 na taarifa 21 za mwenyekiti, na kutoa taarifa 87 kwa vyombo vya habari katika mwaka 2018.

    Ripoti inasema katika mwaka huo, Baraza la Usalama liliendelea kufuatilia migogoro kadhaa mikubwa ambayo haijatatuliwa, haswa katika Mashariki ya Kati na barani Afrika. Inaongeza kuwa athari za migogoro hiyo kwa raia wa kawaida ni kubwa, na misukosuko mikubwa ya kibinadamu iliendelea na baadhi yao imepamba moto zaidi.

    Ripoti imesisitiza kuwa mgawanyiko uliopo katika Baraza la Usalama umelizuia kuchukua hatua zenye ufanisi kutatua baadhi ya migogoro mikubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako