• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Iran ataka vikwazo vya Marekani viondolewe kabla ya mazungumzo

  (GMT+08:00) 2019-09-13 08:54:47

  Rais Hassan Rouhani wa Iran ameitaka Marekani iondoe vikwazo vyake dhidi ya Iran kabla ya kufikiria kuwepo kwa uwezekano wa mazungumzo yoyote. Akizungumza na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron juzi mjini Tehran, rais Rouhani aliikosoa Marekani kwa kukiuka ahadi zake kwenye makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kwa kujitoa kwenye makubaliano hayo Mei mwaka jana. Kiongozi huyo wa Iran pia amesema nchi yake iko tayari kuendelea kutekeleza makubaliano hayo kama makubaliano kati yake na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambazo ni nchi zilizosaini makubaliano ya nyuklia kuhusu utekelezaji wa makubaliano hayo yatatimizwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako