• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mahali atakapozikwa Mugabe kutangazwa kesho

  (GMT+08:00) 2019-09-13 09:36:43

  Msemaji wa familia ya Mugabe Bw. Walter Chidhakwa amesema mahali atakapozikwa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe patatangazwa kesho.

  Kauli hiyo ameitoa jana baada ya rais Emmerson Mnangagwa kuzungumza na mke wa Mugabe kuhusu suala hilo.

  Habari nyingine zinasema maelfu ya wazimbabwe jana walikwenda Uwanja wa michezo wa Rufaro kutoa heshimu zao za mwisho kwa mwili wa Mugabe, ikiwa ni shughuli ya kwanza kati ya shughuli mfululizo za umma za mazishi ya Mugabe zitakazoendelea mpaka Jumamosi.

  Naye makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan jana alikwenda ubalozi wa Zimbabwe nchini China kutoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Mugabe. Bw. Wang amesema Mugabe alitoa mchango mkubwa katika kuhimiza urafiki kati ya China na Zimbabwe na kati ya China na Afrika. China inaenzi urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili, na inaamini watu wa Zimbabwe watapata mafanikio makubwa zaidi chini ya uongozi wa rais wa sasa Emmerson Mnangagwa katika kutimiza utulivu na maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako