• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mafunzo ya Upishi na ukarimu Zanzibar

    (GMT+08:00) 2019-09-13 09:46:54

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi 'Gavu' amesema uamuzi wa Serikali wa kuwaomba washrika wa maendeleo kutoka China kufanya mafunzo ya Upishi na Ukarimu kisiwani Zanzibar, kunatoa fursa ya kutekeleza matakwa ya kisheria na kanuni za Utumishi wa Umma.

    Waziri Gavu amesema hayo katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul wakil katika ufunguzi wa mafunzo ya Upishi na Ukarimu, yanayoendeshwa na Wakufunzi kutoka nchini China.Mafunzo hayo yanayowashirikisha watumishi 45, yatadumu kwa kipindi cha wiki nne, yakiwa na lengo la kuwaongezea ufanisi, uwajibikaji na kuleta tija katika utumishi wa umma. Akizungumza na washiriki wa amafunzo hayo, Gavu alisema mafunzo ya watumishi wa umma ni jambo lililotiliwa mkazo katika sheria ya utumishi wa umma Namba 2 ya mwaka 2011 pamoja na kanuni za utumishi wa Umma za mwaka 2014.

    Mapema, Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar, Xie Xiaowu alisema mafunzo hayo yatawezesha kuwajengea uwezo washiriki, sambamba na kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako