• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi China lamkabidhi Rais Magufuli magari 40 ya JWTZ

  (GMT+08:00) 2019-09-13 09:51:49

  Jeshi la Ukombozi wa watu wa China (PLA) limekabidhi Jeshi la Ulinzi la wananachi wa Tanzania (JWTZ) magari 40 .

  Magari hayo yamepokelewa na Rais John Magufuli ambaye amemshukuru Rais wa China Xi Jinping kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano mzuri wa Tanzania na China ikiwemo misaada ya uwekezaji. Alisema pamoja na kusaidia serikali katika maeneo mbalimbali ya huduma za jamii, ulinzi na usalama, na miundombinu, China ndiyo nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini ikiwa na miradi 723 yenye thamani ya shilingi Trilioni 13.581 na iliyozalisha ajira 87,126.

  Kwa upande wake Luteni Yuanming amemshukuru Rais Magufuli kuhudhuria hafla hiyo, ili kuendeleza na kukuza uhusiano wa nchi hizo ikiwemo uhusiano wa kijeshi na kuhaidi kuwa PLA itaendelea kushirikiana kwa karibu na JWTZ.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako