• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi zinazoendelea zasisitiza tena kuwa maendeleo ni haki muhimu ya binadamu

  (GMT+08:00) 2019-09-13 17:26:03

  Mkutano wa 42 wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa tarehe 11 ulifanya mazungumzo na wajumbe wanaoshughulikia mambo ya haki ya maendeleo.

  Wajumbe wa China wamesema kushikilia kuhimiza na kulinda haki za binadamu kwenye mchakato wa maendeleo ni umaalumu muhimu kwa maendeleo ya haki za binadamu ya China. China imetatua suala la utoaji wa chakula kwa wananchi wake takriban bilioni 1.4, kuwaondoa kwenye umaskini watu milioni 850, kuwapatia watu milioni 770 nafasi za ajira, na kuunda mfumo mkubwa zaidi duniani kwenye sekta za elimu, bima ya matibabu ya raia na hifadhi ya jamii. China pia imetoa pendekezo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kuhimiza Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio na taarifa juu ya "maendeleo yanahimiza mambo ya haki za binadamu".

  Nchi nyingine zinazoendelea ikiwa ni pamoja na Angola, Afrika Kusini, Misri na Pakistan zimesisitiza kuwa haki ya maendeleo ni haki muhimu ya binadamu isiyotengeka, na zimehimiza kuweka haki ya maendeleo iwe na hadhi muhimu zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako