• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Museveni na Uhuru wasaini mkataba wa kuimarisha biashara kati ya jamii za mipakani

  (GMT+08:00) 2019-09-13 19:59:53

  Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemmpongeza mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kusaini mkataba wa kuimarisha biashara kati ya jamii za mipakani za nchini hizo mbili. Yoweri amesema hatua ya rais Kenya ya kusaini mkataba huo ambao unalenga kuboresha biashara kati ya jamii za Karamojong kutoka Uganda na zile za Turkana na Pokot kutoka Kenya.Wakisaini mkataba huo katika wilaya ya Moroto nchini Uganda, marais hao wawili walisema kwa muda mrefu jamii hizo zimekuwa zikipigania mifugo lakini sasa kupitia biashara ghasi hizo zitatoweka.Mkataba huo unakuja wakati ambapo umoja wa mataifa umekuwa ukiendeleza kampeini za kubadilisha ugomvi wa wizi wa mifugo kati ya jamii hizo hadi ule wa kibiashara kwa ajili ya kuimarisha amani mipakani.Baada ya kusaini mkataba huo, rais Museveni ameutaka umoja wa kimataifa kuendeleza kampeini ili kuhakikisha jamii hizo zinajiimarisha kiuchumi ili kuzuia kuingia kwenye desturi ya kuibiana mifugo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako