• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanyabiashara wa Dodoma watakiwa kuchangamkia fursa za mikopo

  (GMT+08:00) 2019-09-13 20:00:15

  Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi ametoa wito kwa wafanyabiashara mjini humo kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha.

  Amesema kwa kufanya hivyo watanufaika na ongezeko kubwa la fursa za kibiashara zinazoibuka katika Jiji hilo ambalo ni makao makuu ya nchi.

  Akizungumza katika uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara ya Benki ya NBC Mkoa wa Dodoma Kunambi mbali na kuipongeza benki hiyo kwa mabadiliko makubwa ya huduma, amesema bado ipo haja kwa wafanyabiashara kuitumia vyema kupata nguvu ya kiuchumi itakayowawezesha kufaidi fursa ya mabadiliko ya ukuaji wa uchumi.

  Ametoa mfano umuhimu wa wafanyabiashara kuwekeza kwenye sekta ya usafiri ambayo kwa sasa Serikali ipo kwenye mpango wa kuondoa gari dogo za abiria maarufu kama vipanya kwenye mizunguko ya mjini ili kutoa fursa kwa magari makubwa kufanya kazi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako