• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema ushirikiano kati ya kusini na kusini ni nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya dunia

  (GMT+08:00) 2019-09-13 20:03:10

  Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun amesema, ushirikiano kati ya kusini na kusini ni nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya dunia nzima. Ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea umeleta nguvu mpya na kuanzisha njia mpya kwa jumuiya ya kimataifa kutimiza ushirikiano wa kunufaishana.

  Bw. Zhang amesema hayo akishiriki mkutano wa kuadhimisha siku ya ushirikiano kati ya kusini na kusini ya Umoja wa Mataifa. Amesisitza kuwa hivi sasa hatua za upande mmoja na ulinzi wa kibiashara zinaendelea kuongezeka, na kuharibu vibaya uhusiano wa kimataifa na kutishia amani na utulivu wa dunia. Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto kubwa katika kupunguza umaskini, ujenzi wa miundombinu na kuboresha maisha ya umma.

  Amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufanya juhudi kuhimiza ushirikiano wa maendeleo ya kimataifa, kujenga mazingira mazuri kwa nchi zinazoendelea, kutekeleza malengo kwa hatua halisi, kujenga uhusiano wa kiwenzi wa dunia, ili kutimiza maendeleo ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako