• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China siku zote yatetea, kutekeleza na kuhimiza shughuli za kuhakikisha haki za binadamu

    (GMT+08:00) 2019-09-14 18:30:18

    Mjumbe maalumu wa wizara ya mambo ya nje ya China anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Bw. Liu Hua amesema, watu wote kunufaika na haki za binadamu ni matumaini ya binadamu wote, na pia ni lengo la Chama cha Kikomunisti cha China, na China siku zote inatetea, kutekeleza na kuhimiza shughuli za kuhakikisha haki za binadamu.

    Bw. Liu ameyasema hayo alipokutana na wanahabari kwenye mkutano wa 42 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Amesema huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na katika miaka 70 iliyopita chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, China imepata mafanikio makubwa katika shughuli za kuhakikisha haki za binadamu. Ameongeza kuwa China imefanikiwa kulisha watu karibu bilioni 1.4, na kuwaondoa watu milioni 850 kutoka kwenye umaskini.

    Bw. Liu amesisitiza kuwa sababu kuu ya China kupata mafanikio makubwa katika mambo ya haki za binadamu, ni kushikilia ujamaa wenye umaalumu wa China, na njia yenye umaalumu wa China katika kuendeleza haki za binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako