• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yathibitisha kuuawa kwa mtoto wa Osama Bin Laden

  (GMT+08:00) 2019-09-15 17:21:35

  Rais Donald Trump wa Marekani amethibitisha kuwa vikosi vya Marekani vilimuua mtoto wa Osama Bin Laden kwenye operesheni ya kupambana na ugaidi.

  Ripoti iliyotolewa na ikulu ya Marekani inasema Hamza Bin Laden aliuawa kwenye operesheni iliyofanyika kwenye mpaka kati ya Afghanistan na Pakistan. Rais Trump amesema kuuawa kwa Hamza Bin Laden anayetuhumiwa na Marekani kupanga na kuwa na uhusiano na makundi kadhaa ya kigaidi, kutapunguza uwezo wa uongozi wa kundi la Al Qaeda na utendaji wake.

  Taarifa hiyo imetolewa baada ya siku ya 18 ya kumbukumbu ya mashambulizi ya Septemba 11. Hamza Bin Laden alichaguliwa kuwa kiongozi wa Al Qaeda mwaka 2015, na mwaka 2017 Marekani ilimtaja kuwa ni gaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako