• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Syria na Russia zafanya mazungumzo juu ya mkutano wa kilele wa pande tatu

  (GMT+08:00) 2019-09-16 08:55:44

  Rais Bashar al-Assad wa Syria jana alikutana na mjumbe maalumu wa rais wa Russia anayeshughulikia mambo ya Syria Bw. Alexander Lavrentiev, na kujadili kuhusu mkutano wa kilele wa pande tatu utakaofanyika leo mjini Ankara.

  Lavrentiev amemtaarifu rais Assad ratiba ya mkutano huo wa kilele kati ya Uturuki, Russia na Iran, pia wamejadili juhudi za Russia za kuondoa vizuizi vilivyowekwa na baadhi ya nchi vyenye lengo la kurefusha vita vya Syria. Amesisitiza kuwa Russia inapenda kuendelea kushirikiana na Syria katika kupambana na ugaidi na kukomboa maeneo yote ya nchi hiyo.

  Mapema siku hiyo Gazati la Syria "al-Watan" lilisema mkutano huo wa pande tatu utajadili mambo mbalimbali yakiwemo hali ya mkoa wa Idlib, ambao ni ngome kuu ya mwisho ya waasi nchini Syria, pamoja na suala la kuunda kamati ya katiba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako