• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shambulizi la droni lasababisha kupungua kwa nusu kwa uzalishaji wa mafuta Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2019-09-16 08:56:07

    Ndege zisizo na rubani juzi zilishambulia maeneo ya Abqaiq na Khurais ya Shirika la mafuta la Saudi Arabia, ambapo shambulizi hilo limesababisha kupungua kwa takriban nusu ya uzalishaji wa mafuta nchini humo.

    Kundi la Houthi la Yemen limetangaza kuhusika na shambulizi hilo. Hata hivyo, Marekani inaishutumu Iran kuongoza shambulizi hilo, kwa kulipatia kundi la Houthi silaha, na kusema Iran inapaswa kuwajibika kutokana na hasara ya Saudi Arabia.

    Shirika la habari la Iran ISNA limeripoti kuwa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Abbas Mousavi jana alijibu tuhuma za Marekani kuwa hazina msingi wowote na hazina maana kabisa. Ameongeza kuwa kusimamisha mashambulizi ya jeshi la muungano dhidi ya Yemen, kupunguza msaada wa kijeshi unaotolewa na nchi za magharibi kwa wavamizi na kutafuta ufumbuzi wa kisiasa ndizo njia pekee za kutatua mgogoro wa Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako