• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza asema atapuuza agizo la bunge la kuahirisha Brexit kama makubaliano na EU hayatafikiwa

    (GMT+08:00) 2019-09-16 09:46:46

    Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson amesema kwenye mahojiano kuwa atapuuza agizo la kuahirisha Brexit kama nchi yake ikishindwa kufikia makubaliano yoyote na Umoja wa Ulaya.

    Akitolea mfano wa mhusika maarufu wa katuni ya Marvel ya Marekani "the Incredible Hulk" Bw. Johnson ameliambia gazeti la Daily Mail kuwa Uingereza itavunja pingu zake kama makubaliano ya Brexit yakishindwa kufikiwa mwishoni mwa mwezi ujao.

    Bw. Johnson amesema Uingereza itakuwa kama Bruce Banner, mwanasayansi mpole ambaye anabadilika kuwa Hulk akikasirika.

    Kwenye mahojiano hayo yaliyofanyika jana Jumapili, Bw. Johnson amesema kama makubaliano yakishindwa kufikiwa na Umoja wa Ulaya, atapuuza agizo lililotolewa wiki iliyopita na Baraza la makabwela la kumtaka aahirishe Brexit hadi Januari 31, mwaka kesho.

    Imefahamika kuwa Bw. Johnson ataelekea Luxembourg leo kuhudhuria mkutano muhimu na mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya Jean-Claude Juncker.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako