• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfuko wa maendeleo ya China na Afrika wawekeza na kuhimiza uwekezaji wa kampuni za China zaidi ya dola za kimarekani bilioni 29

  (GMT+08:00) 2019-09-16 10:35:00

  Habari kutoka Mkutano wa 5 wa baraza la uwekezaji barani Afrika uliofanyika mjini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo zinasema kuwa, mfuko wa maendeleo ya China na Afrika umewekeza dola za kimarekani bilioni 5 katika nchi 36 za Afrika, na kuhimiza kampuni za China kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani bilioni 24 barani humo.

  Mkutano huo liliandaliwa kwa pamoja na wizara ya fedha ya China, benki ya maendeleo ya China, serikali ya Jamhuri ya Kongo na benki ya dunia. Makubaliano ya miradi mbalimbali kati ya China na Afrika yamesainiwa kwenye mkutano huo, ambayo yanalenga kuimarisha zaidi ushirikiano na Afrika katika safari za anga, uzalishaji wa umeme, sekta ya viwanda, sekta ya fedha na kadhalika, na yatasaidia maendeleo endelevu ya uchumi wa Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako