• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China asisitiza usalama na uwazi wa mtandao wa internet

  (GMT+08:00) 2019-09-16 19:44:44

  Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kujenga mazingira ya mtandao yaliyo salama, kusimamiwa kwa urahisi, kufunguliwa na yenye uvumbuzi.

  Alipotoa maelekezo juu ya kampeni ya wiki moja ya usalama wa mtandao wa internet inayofanyika mjini Tianjin, rais Xi amesema ni lazima kutoa mchango kuongeza utimilifu, furaha na usalama wa watu katika mtandao wa internet. Pia amesema, serikali itahakikisha usalama wa habari, haki za kisheria na maslahi ya binafsi kwenye mtandao.

  Rais Xi pia amesema China sio kama tu inatakiwa kuendeleza teknolojia mpya kama akili bandia, muunganiko wa vitu na mitandao ya mawasiliano ya kizazi kipya, bali pia inatakiwa kuongoza maendeleo ya teknolojia kwa sheria na kanuni na viwango vya utawala.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako